Mabalozi Wastaafu wa Tanzania 34 walifanya ziara ya siku 2 jijini Dodoma tarehe 3 na 4 Februari 2020 kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi.

 

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuendelea kutambua mchango mkubwa wa Mabalozi hao kwa nchi katika medani za kimataifa na masuala ya ukuzaji Diplomasia ya Uchumi kwa ujumla. Pia kuendelea kutoa uzoefu wao kwenye masuala ya Diplomasia kwa makundi mbalimbali ikiwemo Wabunge, Wanafunzi na Watumishi wa Wizara.

 

Wakiwa jijini Dodoma Mabalozi hao Wastaafu walipata fursa ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma na Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki zilizopo Mtumba.