Tarehe 04 Julai, 2026. Mheshimiwa  Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania mchini Burundi  alitembelea Shule ya ECOLE DES ELITES CONTEMPORAINES ya Bujumbura lengo likiwa ni kuzindua Klabu ya kiswahili iitwayo BAHATI ikiwa ni moja ya juhudi za kuhamasisha na kukuza matumizi ya Lugha Adhimu ya KISWAHILI nchini Burundi.  Klabu hiyo ina jumla ya watoto  50 ambao walipata wasaa wa kusoma vitabu, hadhi, kuimba mashairi na nyimbo mbalimbali za kiswahili. Katika hatua nyingine Mhe. Ballozi aigawa vitabu mbalimbali vya kiswahili vitakavyo wawezesha watoto kusoma kiswahili na kuwaongezea misamiati. Aidha, alitoa zawadi kwa watoto ikiwa ni njia ya kuhamasisha watoto kupenda kiswahili.
 

  • Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania nchini Burundi akikabidhi vitabu kwa wanafunzi katika kuhamasisha lugha ya kiswahili.
  • Pichani Wanafunzi wa Shule ya ECCO wakifuatilia kwa kariibu uzinduzi wa Klabu ya Kiswahili shuleni hapo.