Tarehe 12 Machi, 2026 Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania nchini Burundi alishiriki Kikao cha Mabalozi wa Afrika kilichofanyika katika Ubalozi wa Tanzania. Katika kikao hicho Mabalozi mbalimbali wa Afrika walishiriki na walijadili masuala mbalimbali yanayojenga ushirikiano. Pamoja na mambo mengine Kikao hicho kilimchagua Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania nchini Burundi kuwa Naibu Dean wa Mabalozi wa Afrika. Vikao hivyo vya Mabalozi hufanyika mara moja kwa mwezi kwa mzunguuko kwa kila Ubalozi.