Tarehe 23 Januari, 2026 Mhe. Evariste Ndayishimiye, Rais wa Jamhuri ya Burundi alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Mhe. Rais Ndayishiye amemteua  Bw. ALfred Haingejeje, Waziri wa Sheria Haki za Binadamu na Jinsia aliyechukua nafasi ya  Bw. Arthemon Katihabwa ambao uteuzi wake umetenguliwa. Aidha, Mhe. Rais amemteua Bw. Damien Nyankuru, Waziri wa Miundombinu Nyumba, Usafirishaji na Vifaa vya Ujenzi aliyechukua nafasi ya  Jean Claude Nzobanaza ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Sherehe za uapisho huo zilifanyika kwenye ukumbi wa Bunge Kigobe.