Tarehe 25 Mei, 2026, Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania nchini Burundi alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Meja, Jenero Aloys Ndayikengurukiye, Gavana wa Mkoa wa Bujumbura. Lengo la mazungumzo hayo ni kujitambulisha kwa Mhe. Gavana, na kumjulisha kuhusu Maonesho ya Biashara  na Utamaduni ya Pamoja Kati ya Tanzania na Burundi(Tanzania and Burundi Joint Expo) ambayo yamepangwa kufanywa na Ubalozi  kuanzia tarehe 21 hadi 24 Mei, 2026.