Tarehe 22 Mei, 2026 ilifanyika "Wine Tasting Festival" Eden Garden Resort mjini Bujumbura iliyoandaliwa na Ubalozi. Lengo la hafla hiyo  lilikuwa ni kuutangaza mvinyo wa Tanzania katika soko la Burundi.
Hafla hiyo iliwakutanisha watengenezaji na wauzaji wa mvinyo kutoka Tanzania, wasambazaji na wauzaji wa mvinyo wa Burundi pamoja na Wanadiplomasia wanaowakilisha nchi na mashirika mbalimbali nchini Burundi.

  • Pichani ni baadhi ya mvinyo (wine) za Tanzania ambazo wageni mbalimbali walipata fursa ya kuonja mvinyo huo zikiwa zimepangwa kitaalamu wakati wa hafla hiyo.
  • Wageni mbalimbali wakifuatilia hafla ya "Wine Tasting Festival"