CRDB bank PLC – Tanzania imewekeza nchini Burundi kuanzia mwaka 2012 kwa kufungua Kampuni tanzu (Subsidiary) mjini Bujumbura, iitwayo CRDB Bank Burundi SA, ambayo ilianza kazi tarehe 02 Novemba 2012. Kampuni hiyo inamilikiwa na CRDB Bank PLC Tanzania kwa asilimia 100. CRDB Bank kwa sasa ina matawi matatu mjini Bujumbura. Aidha, Benki hii kwa sasa inajipanua kwa kuongeza matawi yake katika mikoa mingine ya Burundi. Tarehe 8 Oktoba, 2021 CRDB Bank Burundi ilifungua rasmi tawi lake mkoani Ngozi, mkoa ambao unafuatia kuwa na shughuli nyingi za kibiashara baada ya mkoa wa Bujumbura

  • Mhe. Dkt. Domitien Ndihokubwayo, Waziri wa Fedha, Bajeti na Mpango wa Uchumi wa Burundi (katikati mbele), Mhe. Dkt. Jilly E. Maleko, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, kulia mbele na Bw. Frederick Siwale, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Burundi ( watatu kushoto) wakikata utepe kwenye ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB mkoani Ngozi, Burundi tarehe 08/10/2021
  • Mhe. Dkt. Jilly E. Maleko, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, akitoka hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB mkoani Ngozi, Burundi tarehe 08/10/2021.