Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Uwekezaji wa Norway kwa nchi zinazoendelea (Norwegian Investment Fund for Developing Countries - Norfund), Bw. Tellef Thorleifsson.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Prof. Kabudi pamoja na Bw. Thorleifsson wamejadili masuala yanayohusu fursa za uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Norway.