RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI, MHE. EVARISTE NDAYISHIMIYE, AMEMTUNUKIA NISHANI YA JUU YA HESHIMA, MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KUFUATIA MCHANGO WAKE KATIKA HARAKATI ZA KUREJESHA AMANI NCHINI BURUNDI.
NISHANI HIYO YA HESHIMA ILIPOKELEWA NA BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO, BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI BURUNDI WAKATI WA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU WA BURUNDI ZILIZOFANYIKA TAREHE 01 JULAI, 2020 MJINI BUJUMBURA, BURUNDI.

