Pichani ni Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara za Ujenzi, Uchukuzi, Mawasiliano na Miundombinu wa nchi za Burundi, DRC na Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Burundi, walitembelea Kituo Kikuu cha Reli cha Tanzanite jijini Dar es Salaam.Ujumbe huo ulikuwa unakagua mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa. Ziara hiyo ilifanyika mara baada ya Mawaziri hao kutia saini, makubaliano ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ( SGR kutoka Uvinza (Tanzania) - Gitega (Burundi) - Kindu (DRC) tarehe 7 Machi, 2022.