TAREHE 02 JULAI 2021, BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI, DKT. JILLY E. MALEKO AMEMVISHA CHEO KIPYA BRIGEDIA JENERALI SALUM MNUMBE, KUTOKA KANALI KUWA BRIGEDIA JENERALI. MHE. BALOZI MALEKO AMEMVISHA CHEO HICHO KWA NIABA YA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI. TUKIO HILO LILIFANYIKA KATIKA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI.

BRIGEDIA JENERALI SALUM MNUMBE ALIPANDISHWA CHEO HICHO NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN TAREHE 02 MEI, 2021.