LEO TAREHE 06 MACHI, 2023 TIMU YA YA MAAFISA KUTOKA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA), MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA(TPA) NA SHIRIKA LA UWAKALA WA MELI TANZANIA(TASAC) NA SEKTA BINAFSI (TAFAA, TASAA NA WAMILIKI WA BANDARI KAVU ZA MAGARI )ZINAZOTOA HUDUMA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM, WAMETEMBELEA OFISI ZA UBALOZI NA KUFANYA MAZUNGUMZO MAFUPI NA MHE. BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO, BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI PAMOJA NA MAAFISA WA UBALOZI. TIMU HII IPO NCHINI BURUNDI KWA AJILI YA KUKUTANA NA WAAGIZAJI WA SHEHENA ZA MAGARI (CAR IMPORTERS) KATIKA KIKAO KITAKACHOFANYIKA TAREHE 7 MACHI, 2023, KATIKA HOTELI YA ROYAL PALACE BUJUMBURA, BURUNDI.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly E. Maleko, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, akipokea zawadi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo tarehe 06 Machi, 2023 mara baada ya mazungumzo mafupi na Maafisa hao.
Pichani Mhe. Balozi. Dkt. Jilly E. Maleko. Balozi wa Tanzania nchini Burundi akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wametembelea ofisi za Ubalozi leo tarehe 06 Machi, 2023 na kufanya mazungumzo mafupi na Mhe. Balozi na Maafisa wa Ubalozi.
