MHE. DKT. STERGOMENA TAX, WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, AMEONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA 43 WA KAWAIDA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) ULIOFANYIKA JIJINI BUJUMBURA, BURUNDI TAREHE 23 FEBRUARI, 2023 IKIWA NI MARA YA KWANZA TANGU KUTEULIWA KWAKE WADHIFA HUO. PAMOJA NA AGENDA MBALIMBALI ZILIZOJADILIWA KATIKA MKUTANO HUO ULIJADILI AGENDA MBALIMBALI ZILIJADILIWA NI PAMOJA NA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO MBALIMBALI YALIYOFIKIWA NA BARAZA HILO KWENYE VIKAO VILIVYOPITA; TAARIFA KUTOKA OFISI YA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA PROGRAM MBALIMBALI KATIKA SEKTA ZA MIUNDOMBINU, FORODHA  NA BIASHARA, UTALII NA AJIRA; TAARIFA YA MWAKA YA UKAGUZI WA HESABU ZA JUMUIYA KUANZIA MWEZI JANUARI HADI JUNI 2022 NA RIPOTI YA KAMATI YA UTAWALA NA FEDHA PAMOJA NA KUPITIA NA KUPITISHA RATIBA YA SHUGHULI ZA JUMUIYA KWA KIPINDI CHA KUANZIA MWEZI JANUARI HADI JUNI 2023. KADHALIKA NA MASUALA MENGINE YALIYOJADILIWA NI UMUHIMU WA KUKITANGAZA KISWAHILI DUNIANI KWA KUANZISHA VITUO VYA UTAMADUNI WA LUGHA HIYO KATIKA BALOZI ZA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI; NA KUTOA MWELEKEO WA KUANZA KUTUMIKA KWA LUGHA YA KIFARANSA NA KISWAHILI KATIKA UENDESHAJI WA SHUGHULI RASMI ZA JUMUIYA.

  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stergomena Tax (katikati) akichangia jambo wakati wa Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mhe. Dkt. Tax aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo.
  • Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geophrey Pinda (kulia) akishiriki Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bibi. Amina Khamis Shaaban.
  • Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly E. Maleko akishiriki kikao cha kupokea na kuajdili taarifa ya nchi kilichofanyika kabla ya kuanza Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri.