NCHINI BURUNDI ULIFANYIKA MKUTANO WA 36 WA BARAZA LA KISEKTA LA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA ULINZI WA EAC AMBAO ULIFANYIKA JIJINI BUJUMBURA TAREHE 28 MACHI HADI 01 APRILI 2023. MKUTANO HUO ULIHUDHURIWA NA MAWAZIRI WA ULINZI WA EAC, MAKATIBU WAKUU WA WIZARA, WAKUU WA MAJESHI/ WAWAKILISHI KUTOKA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI. DRC ILISHIRIKI MKUTANO WA NGAZI YA MAWAZIRI TU. AIDHA, BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI MKUTANO HUO PIA. MKUTANO WA BARAZA LA KISEKTA LA USHIARIKIANO KATIKA MASUALA YA ULINZI WA EAC ULIFANYIKA TAREHE 01 APRILI, 2023 ULITANGULIWA NA VIKAO MBALIMBALI VIKIWEMO KIKAO CHA WATAALAMU WA OPERESHENI NA MAFUNZO, KILICHOFANYIKA TAREHE 28 - 29 MACHI, 2023 KIKAO CHA KAMATI YA KISEKTA YA USHIRIKIANO KATIKA ULINZI KILICHOFANYIKA TAREHE 30 MACHI, 2023, PAMOJA NA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA USHIRIKIANO KATIKA ULINZI KILIFANYIKA TAREHE 31 MACHI, 2023.
Pichani: Kutoka Kulia Waziri wa Ulinzi na JKT wa Tanzania Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Waziri wa Ulinzi wa Uganda Mhe. Vincent Bamulangaki Ssempijja, Waziri wa Ulinzi wa Sudan Kusini, Mhe. Chol Thon Balok, Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Mhe, Maj. Gen. Albert Murasira, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Kenya, Mhe. Adan Duale, Naibu Waziri wa Ulinzi wa DRC, Mhe. Samy Adubango Awotho na Waziri wa Ulinzi wa Burundi, Mhe. Eng. Alain Tribert Mutabazi wakiwa tayari kutia saini taarifa ya mkutano tarehe 01 Aprili, 2023.
Pichani Kutoka Kushoto Naibu Waziri wa Ulinzi wa DRC Mhe. Samy Adubango Awotho, Waziri wa Ulinzi na JKT wa Tanzania Mhe. Innocent Lugha Bashungwa na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly E. Maleko, mara baada ya mkutano tarehe 01 Aprili, 2023.