MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA (TCM) KWA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC), ULIFANYIKA KATIKA HOTELI YA ROYAL PALACE BUJUMBURA, BURUNDI KUANZIA TAREHE 6 - 10 FEBRUARI, 2023 NA MASUALA MBALIMBALI YA KISEKTA YALIJADILIWA. MKUTANO HUO ULIHUSISHA NGAZI MBALIMBALI , NGAZI YA WATAALAMU, NGAZI YA MAKATIBU WAKUU NA NGAZI YA MAWAZIRI.
Pichani, Mhe. Balozi. Dkt. Jilly E. Maleko , Balozi wa Tanzania nchini Burundi akisaini taarifa ya Mawaziri ya Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) uliofanyika Bujumbura tarehe 10 Februari, 2023. Mhe. Balozi alishiriki mkutano huo Ngazi ya Mawaziri, akimuwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Tanzania.
