MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA, BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI ALIFANYA ZIARA  SIKU NNE KWENYE JIJI LA MWANZA KUANZIA TAREHE 12-14 JULAI, 2024, NA ALIAMBATANA NA WANAFUNZI KUTOKA VYUO VIKUU MBALIMBALI NCHINI BURUNDI WALIOSHINDA MASHINDANO YA UANDISHI WA INSHA YA LUGHA YA KISWAHILI  YALIYOANDALIWA NA OFISI YA UBALOZI .  LENGO LA ZIARA KWA WANAFUNZI HAO ILIKUWA NI  KUJIFUNZA  KWA KUTEMBELEA  MIRADI MBALIMBALI  YA  UJENZI INAYOENDELEA JIJINI MWANZA. MIRADI WALIYOITEMBELEA NI UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO -  BUSISI , MELI MPYA YA NEW MWANZA HAPA KAZI TU NA KUPATA SAFARI YA MELI KUTOKA MWANZA  KUELEKEA BUKOBA. KUPITIA ZIARA HIYO WANAFUNZI HAO WAMEJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI KUPITIA MIRADI HIYO.

  • MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA, PAMOJA NA WANAFUNZI WAKIPATA MAELEZO KUHUSU UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO, BUSISI.
  • MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA, AKISAINI KITABU CHA WAGENI KABLA YA KUTEMBELEA UJENZI WA MRADI WA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU.
  • MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA, AKIELEZEA LENGO LA KUTEMBELEA UJENZI WA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU NA WANAFUNZI HAO.
  • MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA, AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHINI BURUNDI MARA BAADA YA KUTEMBELEA UJENZI WA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU.
  • MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA, AKIMKABIDHI ZAWADI MHE. SAID MTANDA, MKUU WA MKOA WA MWANZA ALIPOFANYA ZIARA KWENYE OFISI HIYO.
  • MHE. BALOZI AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KISIWA CHA SAA NANE NATIONAL PARK. KATIKA ZIARA HIYO ALIAMBATANA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHINI BURUNDI.
  • MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA PAMOJA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHINI BURUNDI WAKIPEWA MAELEZO KUHUSU KISIWA CHA SAA NANE NATIONAL PARK.