MHE. BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO, BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI AMESHIRIKI KAMA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE YA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ILIYOFANYIKA TAREHE 12 MACHI, 2023 KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA BENKI YA CRDB BURUNDI. SHEREHE HIYO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HUADHIMISHWA KILA MWAKA TAREHE 8 MACHI , AIDHA, BENKI YA CRDB BURUNDI ILIADHIMISHA SHEREHE HIYO TAREHE 12 MACHI, 2023 KWA KUJUMUIKA PAMOJA NA WANAWAKE WENYE AKAUNTI YA MALKIA KWENYE BENKI YA CRDB BUJUMBURA, BURUNDI. AMBAPO WANAWAKE WENGI WAMEFAIDIKA NA AKAUNTI HIYO YA MALIKIA KWA KUWEZA KUFANYA MAENDELEO MBALIMBALI.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly E. Maleko, Balozi wa Tanzania nchini Burundi akihutubia wakati wa sherehe tarehe 12 Machi, 2023.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly E. Maleko, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, akifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea wakati wa sherehe tarehe 12 Machi, 2023.
Mhe. Balozi Dkt. Jilly E. Maleko akitoa zawadi ya mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo tarehe 12 Machi, 2023.