“ Nchini Burundi ninaiona fursa kubwa iliyopo katika sekta ya usafiri na usafirishaji, ipo haja ya TPA na ATCL kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kukuza soko la huduma zinazotolewa na ATCL, pamoja na bandari zetu (TPA).” alisema Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius G. Byakanwa tarehe 15 Novemba, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius G. Byakanwa akiwa na Mwakilishi wa Ofisi ya TPA Bujumbura, Bw. Emmanuel Nkumbi, na Mwakilishi wa Ofisi ya ATCL Bujumbura, Bi. Harrieth Rutihinda tarehe15 Novemba, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius G. Byakanwa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa Ofisi ya TPA Bujumbura, Bw. Emmanuel Nkumbi na Wafanyakazi wa TPA tarehe15 Novemba, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius G. Byakanwa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank S.A Bujumbura, Bw. Fredrick Siwale na Wafanyakazi wa benki hiyo tarehe15 Novemba, 2023.
