Tarehe 19 Mei, 2024 kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Balozi Gelasius G. Byakanwa, alifanya makabidhiano ya ndege wanne aina ya Tausi ikiwa ni zawadi kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ikulu ya Gitega, Burundi. Baada ya makabidhiano Rais wa Burundi alishukuru sana na kusema yafuatayo:-
“Rais Samia Suluhu Hassan ni rafiki yangu, mimi namwita dada yangu naye anaiita kaka yake. Urafiki wetu huu umeendelea kuimarisha urafiki wa nchi zetu mbili. Watanzania na Warundi ni ndugu. Nimefurahi sana kupokea ndege hawa wazuri nitawatunza na kuhakikisha wanazaliana na kuongezeka. Fikisheni shukrani zangu kwa dada yangu”.
BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI AKABIDHI NDEGE WANNE AINA YA TAUSI KWA RAIS WA BURUNDI.
MHE. GELASIUS G. BYAKANWA, BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI AKISALIMIANA NA MHE. EVARISTE NDAYISHIMIYE, RAIS WA BURUNDI KATIKA IKULU YA GITEGA, BURUNDI KABLA YA MAKABIDHIANO YA NDEGE WA NNE AINA YA TAUSI.
(1)_1000_1000shar-50brig-20.jpg)