TAREHE 10 .7. 2025 UBALOZI ULIADHIMISHA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI YALIYOFANYIKA CHUO KIKUU CHA MUTANGA NCHINI BURUNDI. KATIKA MAADHIMISHO HAYO WALISHIRIKISHWA WANAFUNZI THELATHINI (30) KUTOKA VYUO VIKUU VINAVYOFUNDISHA KISWAHILI NCHINI BURUNDI NA KUSHINDANISHWA KWENYE MADA TATU INSHA, MASHAIRI,NA MDAHALO KWA MADA ISEMAYO "KISWAHILI NDIO UTAMBULISHO WA MWAFRIKA". MAADHIMISHO HAYO YALILENGA KUPATA NA KUJUA UWEZO WA WANAFUNZI KATIKA UANDISHI WA LUGHA YA KISWAHILI. PAMOJA NA MAMBO MENGINE UBALOZI ULITOA ZAWADI KWA WASHINDI WOTE NA MWISHO WALIPATIKANA WASHINDI WATATU KWA KILA KUNDI UANDISHI WA INSHA, MASHAIRI NA MDAHALO.