Leo tarehe 31.7.2025 Kambi ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali Benjamin Mkapa kutoka Dodoma  iliyokuwa inatoa huduma ya matibabu kwenye Hospitali ya Prince Regent Charles jijini Bujumbura imefungwa rasmi. Mgeni rasmi alikuwa Mke wa Rais wa Burundi Mhe. Angeline Ndayishimiye.

  • Mke wa Rais wa Burundi, Mhe. Angeline Ndayishimiye akipokea maelezo mafupi kuhusu kambi hiyo.
  • Watu mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali.
  • Mke wa Rais wa Burundi, Angeline Ndayishimiye akimjulia hali mtoto aliyepata huduma ya matibabu kutoka kwa madaktari bingwa.
  • Madaktari wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ufungaji wa kambi ya matibabu.