Tarehe 23.10.2025 Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Burundi alifanya mazungumzo na Mhe. Balozi Edouard Bizimana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Burundi ambaye amechaguliwa hivi karibuni kwa lengo la kujitambulisha na walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania nchini Burundi akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Edouard Bizimana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Burundi kwenye ofisi ya wizara hiyo.
Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania nchini Burundi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Edouard Bizimana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Burundi na watendaji wengine wa wizara hiyo.
