Orbit Securities Tanzania imefungua rasmi kampuni tanzu Orbit Investment Bank Burundi, ikiwa ni hatua kubwa katika kupanua huduma za uwekezaji Afrika Mashariki. Hafla ya uzinduzi huu imefanyika mjini Bujumbura na kuhudhuriwa na wageni mashuhuri akiwemo, Mgeni rasmi, Mh. Gelasius G. Byakanwa, Balozi wa Tanzania nchini Burundi; Bw. Robert Mathew, CEO wa Burundi Securities Exchange (anayejulikana kwa mchango wake mkubwa wa kuanzisha masoko ya hisa Dar es Salaam, Uganda, Rwanda na Burundi); Bw. Arséne Mugenzi, CEO wa CMSA (ARMC) Burundi; pamoja na viongozi wa mabenki makubwa ya biashara na mifuko ya uwekezaji ya hifadhi ya jamii.

Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Burundi pia alihudhuria tukio hili adhimu.

Bw. Godfrey Malauri, CEO wa Orbit Securities na Mwenyekiti wa Orbit Investment Bank Burundi, alisema:
"Huu ni mwanzo mpya wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Burundi. Tumejipanga kutoa huduma bora na bunifu zitakazochochea ukuaji wa soko la mitaji na uchumi wa Burundi."

Tunajivunia hatua hii muhimu na tunatarajia kuleta mageuzi chanya kwenye sekta ya fedha Burundi!

  • Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea katika uzinduzi huo.