LEO TAREHE 15 .7.2025 UMEFANYIKA UFUNGUZI WA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA KUTOKA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA DODOMA. UFUNGUZI HUO UMEFANYIKA MKOANI GITEGA NA MGENI RASMI ALIKUWA WAZIRI WA AFYA BURUNDI, DKT. BARADAHANA LYDWINE. KAMBI HIYO IPO NCHINI BURUNDI  TAREHE 14-25 JULAI, 2025 KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA ZA AFYA MUHIMU KWA RAIA WA BURUNDI WENYE UHITAJI MKUBWA WA HUDUMA HIZO. MATARAJIO YA KAMBI HIYO NI KUPATA WAGONJWA WATAKAOPENDA KUPATA MATIBABU  KATIKA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA DODOMA. HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA NI : MIFUPA YA AJALI(ORTHOPEDICS AND TRAUMATOLOGY), UPASUAJI WA UBONGO, MISHIPA YA FAHAMU,NA UTI WA MGONGO(NEUROSURGERY),MAGONJWA YA MFUMO WA MKOJO(UROLOGY),MAGONJWA YA DAMU NA UPANDIKIZAJI ULOTO(BONE MARROW TRANSPLANT AND HAMATOLOGICAL DISEASES), MAGONJWA YA MOYO(CARDIOLOGY),MAGONJWA YA FIGO NA UPANDIKIZAJI FIGO(NEPHROLOGY), UPASUAJI(GENERAL SURGERY),MAGONJWA YA MACHO(OPHTHALMOLOGY ) NA HUDUMA YA UTOAJI DAWA YA USINGIZI.

  • WANANCHI MBALIMBALI WAKIFUATILIA KWA KARIBU UFUNGUZI WA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA.