TAREHE 7 NOVEMBA , 2024 MHE. GELASIUS G. BYAKANWA ALIMTEMBELEA WAZIRI WA ULINZI WA BURUNDI, MHE. ENG. ALAIN T. MUTABAZI. LENGO YA ZIARA HIYO NI KUJITAMBULISHA NA KUFANYA MAZUNGUMZO MAFUPI KUHUSU USHIRIKIANO WA TANZANIA NA BURUNDI KWENYE MASUALA YA ULINZI. MAONGEZI HAYO YALIJIKITA KWENYE MCHAKATO WA KUKAMILISHA MoU. ALIELEZA KUWA MCHAKATO UMEKAMILIKA NA BURUNDI WAKO TAYARI KUSAINI MAKUBALIANO HAYO.AIDHA, ALIELEZA KUWA WANAPENDEKEZA MAKUBALIANO HAYO YASAINIWE NCHINI TANZANIA.