KUANZIA TAREHE 4 -6 NOVEMBA, 2024 CLOUDS TV WALIFANYA MAHOJIANO YA LIVE KUHUSU TATHMINI YA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA KATI YA TANZANIA NA BURUNDI KWA KIPINDI CHA MIAKA 20 KWENYE OFISI YA UBALOZI. MAHOJIANO NAYO ILIJUMUISHA TAASISI ZA SERIKALI YA TANZANIA ZILIZOPO NCHINI BURUNDI, ATCL, CRDB BENKI NA TPA PAMOJA NA WADAU WANAZOZITUMIA TAASISI HIZO.PAMOJA NA MAMBO MENGINE CLOUDS TV WALIPATA FURSA YA KUFANYA MAHOJIANO NA VIONGOZI WA SERIKALI YA BURUNDI NA WAFANYABIASHARA MBALIMBALI AMBAO WANANDOTO YA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA.