TAREHE 16.8.2025 TANZANIA NA BURUNDI ZILIWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) INAYOZIUNGANISHA NCHI MBILI KWA KIPANDE CHA UVINZA - MSONGATI YENYE UREFU WA KILOMITA 300 AMBAPO KILOMITA 240 KATI YA HIZO NI NJIA KUU NA KILOMITA 60 NI NJIA ZA KUPISHANA. SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI ZILIFANYIKA NCHINI BURUNDI ENEO LA UJENZI MSONGATI. SHEREHE HIZO ZILIHUDHURIWA NA MAMIA YA WARUNDI WAKIONGOZWA NA MHE. EVARISTE NDAYISHIMIYE, RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI PAMOJA NA MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA MAJALIWA, WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIYEMWAKILISHA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. MSAFARA KUTOKA TANZANIA ULIJUMUISHA PIA BAADHI YA MAWAZIRI AMBAO NI:- WAZIRI WA UCHUKUZI WA TANZANIA, MHE. PROF. MAKAME MBARAWA, WAZIRI WA FEDHA, MHE. MWIGULU NCHEMBA, WAZIRI WA MAJI, MHE. JUMA AWESO, WAZIRI WA ELIMU, PROF. ADOLF MKENDA, WAZIRI WA ELIMU WA ZANZIBAR, MHE. LELA MOHAMMED MUSSA, NA WAZIRI WA UJENZI, MHE. ABDALLAH ULEGA. KWA UPANDE WA BURUNDI KULIKUWEPO PIA MAKAMU WA RAIS WA BURUNDI, MHE. PROSPER BAZOMBANZA, WAZIRI MKUU, MHE. NESTOR NTAHONTUYE, WAZIRI WA UCHUKUZI, MHE. JEAN CLAUDE NZOBANEZA, WAZIRI WA ULINZI, MHE. MARIE CHANTAL NIJIMBERE NA CHIEF CABINET/ KATIBU MKUU KIONGOZI NA KATIBU MKUU WA CHAMA TAWALA CNDD-FDD, GENERAL REVERIEN NDIKURIYO PAMOJA NA WATENDAJI WENGINE WENGI WA SERIKALI. MHE. MAJALIWA AKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO AMEMSHUKURU RAIS WA NDAYISHIMIYE KWA MAPOKEZI MAZURI NA UKARIMU ALIOUONESHA KWA UMAKINI WA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO ILI UKAMILIKE KWA WAKATI NA KUFANIKISHA MALENGO YALIYOWEKWA, ALIMALIZIA KWA KUSEMA "UTEKELEZAJI WA MRADI HUU NI MATUNDA YA USHIRIKIANO WA KIHISTORIA KATI YA NCHI ZETU ULIOANZISHWA MWAKA 1975 NA KUIMARISHWA KUPITIA MIKUTANO YA TUME YA PAMOJA YA KUDUMU"
MHE. KASSIM MAJALIWA , WAZIRI MKUU WA TANZANIA NA RAIS WA BURUNDI MHE. EVARISTE NDAYISHIMIYE WAKICHANGANYA UDONGO WAKATI WA HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI.
MHE. GELASIUS G. BYAKANWA, BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MHE. KASSIM MAJALIWA, WAZIRI MKUU WA TANZANIA WAKATI WA HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI.
MHE. KASSIM MAJALIWA, WAZIRI MKUU WA TANZANIA AKIHUTUBIA WAKATI WA HAFLA YA UWEKAJII WA JIWE LA MSINGI.
MHE. EVARISTE NDAYISHIMIYE, RAIS WA BURUNDI AKIHUTUBIA WAKATI WA HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI.