TAREHE 07 NOVEMBA, 2022 MHE. BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO ALIKUTANA NA MHE. GERVAIS NDIRAKOBUCA, WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA BURUNDI . LENGO LA ZIARA HIYO LILIKUWA NI KUMPONGEZA WAZIRI MKUU KWA KUTEULIWA KWAKE KUSHIKA NAFASI HIYO NA KUJADILIANA MAENEO YA USHIRIKIANO BAINA YA TANZANIA NA BURUNDI. MHE. BALOZI ALITUMIA NAFASI HIYO KUWASILISHA SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA KWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA, MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA NA MHE. NDIRACOBUCA ALISHUKURU SANA KUPOKEA SALAMU HIZO NAYE ALIWASILISHA SALAMU ZAKE KWA MHE. MAJALIWA. KATIKA ZIARA HIYO MHE. BALOZI ALIAMBATANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA CRDB BANK BURUNDI S.A, BW. FREDRICK SIWALE KWA LENGO LA KUTOA MWALIKO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA CRDB BANK BURUNDI S.A TOKA KUANZISHWA KWAKE NCHINI BURUNDI.
MHE. BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MHE. GERVAIS NDIRAKOBUCA ,WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA BURUNDI.
