MHE. BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO ALIFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA BUKAVU, KIVU KUSINI-DRC  KUANZIA TAREHE 27 - 30 APRILI, 2023 AKIWA AMEAMBATANA NA CRDB BANK S.A BURUNDI, TPA BURUNDI, VIONGOZI WA TCCIA KAGERA. WAKATI AKIWA KWENYE ZIARA HIYO MHE. BALOZI ALIPATA FURSA YA KUMTEMBELEA MHE. THĖO NGWABIDJE KASI,  GAVANA WA JIMBO LA  KIVU KUSINI NCHINI JAMHURI YA DEMOKRASIA YA KONGO - DRC ,NA KUFANYA NAE MAZUNGUMZO MAFUPI, MASOKO YA BIDHAA NA MAZAO PIA KUHUDHURIA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA BIASHARA. KONGAMANO HILO LIMELENGA KUTAFUTA MASOKO YA HUDUMA ZA TAASISI ZA TANZANIA PAMOJA NA MASOKO YA BIDHAA ZA VIWANDANI NA MAZAO YA KILIMO YA TANZANIA NCHINI DRC. AIDHA USHIRIKI WA TPA  BURUNDI KATIKA KONGAMANO HILO ULIKUSUDIA KUKUTANA NA WASAFIRISHAJI WA BIDHAA KWA NJIA YA MAJI WA JIMBO LA KIVU KUSINI NA KUPATA MAONI YAO KUHUSU  HUDUMA ZA BANDARI ZITOLEWAZO NA TPA.

  • MHE. BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO AKICHANGIA MADA WAKATI WA UZINDUZI WA 2023 BUKABU - KAGERA BUSINESS FORUM TAREHE 29 APRILI, 2023.
  • MHE. BALOZI DKT. JILLY E. MALEKO AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MHE. SAID JUMA MSHANA, BALOZI WA TANZANIA NCHINI DRC WAKINAKILI JAMBO WAKATI WA KIKAO CHA PAMOJA KATI YA MHE. GAVANA WA MKOA WA KIVU KUSINI NA WATENDAJI WAKE NA UJUMBE WA TANZANIA (TCCIA)KAGERA, OFISI YA TPA NA CRDB BANK BURUNDI .
  • MHE. BALOZI DKT. JILL E. MALEKO AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MHE. THĖO NGWABIDJE KASI, GAVANA WAJIMBO LA KIVU KUSINI NCHINI JAMHURI YA DEMOKRASIA YA KONGO - DRC NA MHE BALOZI SAID JUMA MSHANA BALOZI WA TANZANIA NCHINI DRC, WALIPOTEMBELEA MAONESHO YA BIDHAA YA KITANZANIA NA DRC WAKATI WA KONGAMANO.