Kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Burundi uliandaa maonesho ya "Wiki ya Ijue Tanzania", yakiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Ubalozi uliandaa mabanda ya maonesho 40 katika viwanja vya Itwari Mjini Bujumbura ambayo yalitumiwa na makampuni na wajasiliamali mbalimbali kutoka Tanzania na Burundi. 

Walioshiriki maonesho hayo ni Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Bujumbura, Taasisi za Serikali ya Tanzania ambazo ni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya ya Mbuga za Wanyama (TANAPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Yalikuwepo pia Makampuni ya Wafanyabiashara Wakubwa Burundi ambayo ni, CRDB Bank S.A Burundi, FOMI, AZANIA Grain Milling Company, AZAM Bakhresa Milling Grain, Taifa Gas, Msumba Steel, Afritextile, SAFIBU), Wajasiliamali 15 kutoka mkoa wa Kagera  chini ya uratibu wa TCCIA Kagera, Kigoma mmoja (Deus Vumi Kigoma), TAWICO (mvinyo) Dodoma, wajasiliamali kutoka Burundi idadi 12, pamoja na Jumuiya ya Watanzania waishio Burundi (JUTABU).

 

Maonesho ya "Wiki ya Ijue Tanzania" Bujumbura yalianza tarehe 06 – 09 Disemba 2021. Aidha, sherehe za uzinduzi rasmi zilifanyika tarehe 07 Disemba 2021 na mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi Mheshimiwa Balozi Ezechiel NIBIGIRA , Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi. Maonesho hayo yalifungwa rasmi tarehe 09 Disemba 2021 katika sherehe ambazo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania Burundi Mheshimiwa Dkt. Jilly Maleko. Aidha, yaliambatana na shindano la lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Burundi, lililokuwa na mada "Chimbuko la lugha ya Kiswahili na jinsi kilivyoimarisha mahusiano kati ya nchi rafiki za Tanzania na Burundi". Shindano hilo liliratibiwa na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania hapa Burundi, Chuo Kikuu cha Burundi, pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, zawadi kwa washindi wa watatu zilitolewa.

Maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania yalitoa nafasi kuitangaza Tanzania hususan katika nyanja za Utalii, Viwanda, Biashara, Kilimo, Ufugaji, Miundombinu, pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Tanzania. Wageni mbalimbali walitembelea maonesho hayo wakiwemo Viongozi wa Serikali ya Burundi, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Burundi, pamoja na wakazi wa Bujumbura na mikoa ya jirani. Washiriki wa maonesho walitumia fursa hiyo kuzitangaza bidhaa na huduma zinazotolewa na taasisi husika mbalimbali zilizohudhuria, na kuyafanya maonesho yafane na kutimiza lengo lililokusudiwa.

 • Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Dkt. Jilly E. Maleko akishuhudia Balozi wa Uturuki nchini Burundi akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Maonesho la Ubalozi
 • Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt. Jilly E. Maleko akimkabidhi zawadi Balozi wa Misri Nchini Burundi alipotembelea Banda la Ubalozi wakati wa Maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania
 • Mheshimiwa Balozi Dkt Jilly Maleko akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi Mhe. Balozi Ezechiel NIBIGIRA , Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi katika Uzinduzi wa Wiki ya Ijue Tanzania
 • Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Dkt. Jilly E. Maleko akitia Saini kitabu cha Wageni cha wajasiriamali kutoka Mkoa wa Kagera walioshiriki maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania hapa Burundi
 • Mheshimiwa Balozi Dkt. Jilly E. Maleko akitoa zawadi kwa Mgeni Rasmi Mhe. Balozi Ezechiel NIBIGIRA , Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi alipotembelea Banda la Ubalozi tarehe 07 Disemba, 2021
 • Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko (wa pili kutoka kulia ) akiwa na Mgeni Rasmi Mhe. Balozi Ezechiel NIBIGIRA, Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi (katikati) siku ya uzinduzi wa Wiki ya Ijue Tanzania wakiwa na Makatibu Wakuu, Meya wa Bujumbura na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Burundi, mara baada ya sherehe za uzinduzi tarehe 07 Disemba, 2021
 • Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko akiwa na Mgeni Rasmi Rasmi Mhe. Balozi Ezechiel NIBIGIRA , Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi wakitembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania hapa Burundi tarehe 07 Disemba, 2021
 • Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko (waliokaa wa pili kulia) akiwa na Mgeni Rasmi Mhe. Balozi Ezechiel NIBIGIRA , Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi katika uzinduzi wa Wiki ya Ijue Tanzania (waliokaa wa tatu kulia), Makatibu Wakuu, Meya wa Bujumbura, pamoja na Washiriki wa Shindano la Lugha ya Kiswahili mara baada ya washindi kuzawadiwa tarehe 07 Disemba, 2021
 • Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko akiwa na akiwa na Kikundi cha Ngoma za Kirundi siku ya Uzinduzi wa Wiki ya Ijue Tanzania tarehe 07 Disemba, 2021
 • Wakazi wa Bujumbura wakitembelea Mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania
 • Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko akimpatia zawadi Balozi wa DRC alipotembelea banda la Ubalozi tarehe 07 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko akiwa na akiwa na na Wajasiliamali kutoka Mkoa wa Kagera , mara baada ya kuwakabidhi vyeti vya ushiriki wa maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania tarehe 09 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko (aliyevaa gauni la kitenge), Balozi wa Nigeria (kulia kwa Balozi wa Tanzania), Mke wa Balozi wa Nigeria (kushoto kwa Balozi wa Tanzania) akiwa na baadhi ya Watanzania waishio Burundi (JUTABU), Wiki ya Ijue Tanzania tarehe 09 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko akikabidhi cheti cha ushiriki wa Maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania kwa mshiriki kutoka mkoa wa Kagera tarehe 09 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko anaonekana akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Burundi Bw. Frederick Siwale katika Banda la Ubalozi tarehe 08 Disemba, 2021
 • Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Jeshi la Burundi Brigedia Jenerali Baratuza Gaspard akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Ubalozi wakati wa maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania tarehe 07 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Dkt Jilly Maleko akimkabidhi cheti cha ushiriki mjasiliamali wa Kirundi tarehe 09 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Dkt. Jilly E. Maleko akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaendeleo wa Burundi Bw. Ferdinand BASHIKAKO mara baada ya kumpatia zawadi Balozi alipotembelea banda la Ubalozi tarehe 07 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi Dkt. Jilly E. Maleko akiwa na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Burundi walioshiriki kama Wasaidizi (ushers) wakati wa maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania
 • Mheshimiwa Balozi Dkt. Jilly E. Maleko akihutubia kuhitimisha Wiki ya Ijue Tanzania tarehe 09 Disemba, 2021
 • Mheshimiwa Balozi Dkt. Jilly E. Maleko akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhitimisha Wiki ya Ijue Tanzania tarehe 09 Disemba, 2021
 • Kikundi cha Taarabu kikitoa burudani mara baada ya Mheshimiwa Balozi wa Tanzania kuhitimisha maonesho ya Wiki ya Ijue Tanzania tarehe 09 Disemba, 2021