TAREHE 16 JANUARI, 2023 MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA  AMEKUTANA NA MHE. MBULELO BUNGANE, BALOZI WA AFRIKA KUSINI NCHINI BURUNDI. HII NI MARA YA KWANZA KWA MHE. BALOZI ANAMPOKEA BALOZI MWENZAKE OFISINI KWAKE TANGU ARIPOTI KITUO CHA BUJUMBURA MWEZI OKTOBA, 2023.

"TANZANIA IMEKUWA MSTARI WA MBELE WAKATI WA HARAKATI ZA UKOMBOZI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA, ITAKUWA VYEMA HISTORIA HIYO IANDIKWE ILI VIZAZI VIJAVYO WAIJUE NA KUISHI NA MAONO YA VIONGOZI WETU HUSUSAN MWL. JULIUS NYERERE NA MZEE NELSON MANDELA" ALISEMA MHE. BALOZI WA AFRIKA KUSINI.

‘’AFRIKA KUSINI NA TANZANIA TUMEKUWA TUKISHIRIKIANA KATIKA NYANJA MBALIMBALI, UWEPO WA BALOZI ZETU HAPA BUJUMBURA IWE NI SEHEMU YA KUDUMISHA USHIRIKIANO WENU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI ZETU NA "SADC" ALISEMA MHE. BALOZI BYAKANWA.

  • MHE. BALOZI GELASIUS G. BYAKANWA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MHE. MBULELO BUNGANE, BALOZI WA AFRIKA KUSINI NCHINI BURUNDI BAADA YA MAZUNGUMZO MAFUPI ALIPOKUJA KUTEMBELEA OFISI YA UBALOZI KWA LENGO LA KUJITAMBULISHA TAREHE 16 JANUARI, 2024.